TADB Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano na Wizara ya Kilimo

 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw.Frank Nyabundege amefanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo, katika kikao maalum kilicholenga kujitambulisha na kuimarisha ushirikiano kati ya benki ya TADB na Wizara ya Kilimokuimarisha ushirikiano kati ya benki ya TADB na Wizara ya Kilimo.



Katika kikao hicho, Waziri Chongolo aliipongeza TADB kwa ufanisi wake katika uendeshaji wa shughuli zake pamoja na mchango wake katika kuchochea maendeleo jumuishi na endelevu katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo nchini.

Vilevile katika mazungumzo hayo, ujumbe wa benki uliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TADB, ikiwemo mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka kumi hasa katika kuchagiza mageuzi ya sekta ya kilimo kuelekea kilimo cha kibiashara.




Aidha, Waziri Chongolo alitoa maelekezo kwa benki hiyo kuhusu maeneo mbalimbali yanayohitaji kuongezewa juhudi ili kuimarisha zaidi utoaji wa huduma kwa wakulima pamoja na wadau wa biashara za kilimo nchini.



Kwenye kikao hicho pia alikuwepo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TADB, Bi.Afia Sigge, kama sehemu ya ujumbe wa benki.


Previous Post Next Post