Katika kutekeleza dhamira hiyo, TADB imetoa pembejeo za kilimo kwa kikundi hicho, kinachojishughulisha na uzalishaji wa mpunga, matunda na mbogamboga kwa lengo la kuongeza tija ya uzalishaji, kuinua kipato cha wanachama, pamoja na kuimarisha usalama wa chakula katika jamii.
Uwezeshaji huu ni sehemu ya mkakati mpana wa TADB wa kukuza ushiriki wa wanawake katika mnyororo wa thamani wa kilimo, sambamba na kuchochea maendeleo ya kiuchumi vijijini.
Kupitia jitihada hizi, TADB inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kutambua na kuimarisha mchango wa wanawake kama nguzo muhimu katika maendeleo ya sekta ya kilimo na uchumi wa taifa kwa ujumla.