TADB YAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WAKULIMA MKOANI RUVUMA










Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeendelea na juhudi zake za kuwawezesha wakulima kupitia mafunzo ya uelewa kuhusu huduma na bidhaa zake kwa wakulima 120 kutoka Wilaya za Songea Mjini, Songea Vijijini, Namtumbo pamoja na Madaba mkoani Ruvuma




Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Brig. Gen. Ahmed Abbas Ahmed, ambaye aliwahimiza washiriki kutumia maarifa waliyopata kuboresha uzalishaji, kuongeza tija, na kuimarisha ufanisi katika shughuli zao za kilimo-biashara.


Miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Huduma za TADB, Urasimishaji wa kilimo-biashara, Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS), Hali ya kilimo, ufugaji na uvuvi katika Wilaya ya Songea Mjini na Uimarishaji wa vyama vya ushirika na AMCOS.


Wakulima walioshiriki walitoa shukrani zao kwa TADB kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu, wakisisitiza kuwa yamewaongezea uelewa juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo na jinsi wanavyoweza kunufaika nazo ili kukuza shughuli zao za kilimo-biashara.



Previous Post Next Post