TADB imeendelea kuonyesha uthubutu wake katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, ikilenga kuimarisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira na kukuza uendelevu wa kilimo nchini
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi, amekutana na ujumbe wa TADB ukiongozwa na Mkurugenzi wa Mipango,Ushauri na Ushirikiano wa Taasisi Bw. Mkani Waziri na kujadili kuhusu mbinu za kuendeleza ushirikiano katika masuala ya mazingira.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda, pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Mabadiliko ya Tabianchi na Tathmini ya Mazingira, Dkt. Kaniziro Manyika na kwaupande wa TADB pia alikuwepo Afisa Mwandamizi Mipango na Mabadiliko ya Tabianchi, Bi. Hawabai Abdulla.




